Halmashauri ya ukusanyaji ushuri nchini KRA imerudisha magari mane kati ya 21 yanayoaminika kuibwa kutoka nchini Uingereza na kuingia humu nchini kupitia Bandari ya Mombasa kati ya mwezi Machi hadi Septemba mwaka huu.
Akizungumza mjini Mombasa wakati wa kukagua makasha yaliyokuwa yamebeba magari hayo kabla ya kupakiwa na kurudishwa Marekani kamishna wa uchunguzi wa KRA Dr. Terra Saidimu amedai kutia bidii zaidi katika kuhakikisha Bandari ya Mombasa haipitishi bidhaa kinyume cha sheria.
Wakati uo huo ametoa wito kwa asasi husika kushirikiana katika kukabiliana na visa kama hivyo kikamilifu.