Mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini KRA imeyanasa magari matano ambayo yameingizwa humu nchini kutoka nchini Uingereza kupitia bandari ya Mombasa kinyume cha sheria.
Magari hayo aina ya Range Rover Vogue, Range Rover Sport, BMW 53D, BMW X5, na Vox Wagen w53d yanadaiwa kuibiwa kati ya mwaka wa 2018/2019.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Mratibu wa KRA, Kenneth Ochola amesema wakati wa oparesheni hiyo pia walifanikiwa kunasa pikipiki mbili zilizoingizwa humu nchini kimagendo.
Ochola amedokeza kuwa magari ambayo yamenaswa yalikuwa yameidhinishwa kusafirishwa nchini Uganda, lakini kupitia ushirikiano wa pamoja wa maafisa wa polisi wa Kenya, Uingereza na maafisa wa polisi wasio kuwa na mipaka wamefakiwa kuyanasa magari hayo.