.
Kikosi cha ulinzi wa baharini (KCGS) kimepokea rasmi boti la kuimarisha usalama majini kutoka kwa halmashauri ya kukusanya ushuru nchini KRA lililogarimu takriban shilling milioni 90.
Akiongea katika ufuo wa bahari ya mnarani kwa niaba ya kamishina generali wa halmashauri hiyo Daktari Fred Mugambi amesema boti hiyo itaweza kukabiliana vilivyo na usafirishaji wa bidhaa gushi, bidhaa haramu,madawa ya kulevya pamoja na ugaidi.
Mugambi amesema kifaa hicho pia kitaimarisha biashara za baharini ambazo ndio tegemeo kubwa la uchumi nchini.