Story by Bakari Ali–
Halmashauri ya bandari nchini KPA imeahidi kutekeleza miradi ya maendeleo ya jamii katika kaunti ya Taita taveta na kwengineko Pwani ili kuhakikisha jamii inanufaika na shughuli za bandari hiyo.
Akizungumza mjini Voi katika kaunti ya Taita Taveta, Kaimu mkurugenzi mkuu wa Halmashauri hiyo John Mwangemi amesema miradi kama ile ya elimu na afya imepewa kipau mbele na Halmashauri hiyo.
Mwangemi ameiahidi jamii kwamba Halmashauri hiyo itafanya kazi na jamii mashinani katika juhudi za kuimarisha hali yao ya maisha.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya Priscillah eneo la Voi Peninah Mwanjala, iliyonufaika na ufadhili wa shilingi milioni moja ili kufanikisha ujenzi wa afisi amekiri kuwepo na changamoto katika sekta ya elimu huku akiishukuru halmashauri hiyo kwa msaada huo.
Shule nyingine zilizonufaika na ufadhili huo ni pamoja na shule ya msingi ya Kalela iliyopata shilingi milioni 4 sawa na shule ya msingi ya Kale iliyopata shilingi milioni 2, fedha ambazo zitaboresha miundo msingi shuleni.