Story by: Mwahoka Mtsumi
Halmashauri ya bandari nchini KPA imesambaza chakula cha msaada kwa zaidi ya familia elfu moja katika vijiji vya Ndavaya na Lutsangani kwenye gatuzi dogo la Kinango kaunti ya Kwale wanaokabiliwa na uhaba wa chakula na maji.
Akizungumza na Wanahabari wakati wa ugawa wa chakula hicho kwa wahanga wa njaa, Mwenyekiti wa KPA Benjamini Dalu Tayari amesema chakula hicho kimegharimu shilingi milioni 1.5 na juhudi hizo zitaendelezwa kuwasaidia wale wenye uhitaji zaidi.
Tayari amedai kwamba baadhi ya maeneo ya gatuzi dogo la Kinango bado ni kame kutokana na ukosefu wa mvua kwa mda mrefu, akisisitiza haja ya wahisani mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wakaazi hao wanaopitia hali ngumu ya kiuchumi.
Wakati uo huo ameeleza kwamba Halmashauri ya bandari nchini KPA inashirikiana kwa karibu mno na serikali kuu na zile za kaunti ambazo zinashuhudia hali ngumu ya ukame ili kuibuka na mikakati ya kutatua changamoto hizo.