Story by Bakari Ali –
Halmashauri ya bandari nchini KPA imepokea mashine 3 za thamani ya shilingi bilioni 3.3 za kupakia na kupakua shehena katika bandari ya Mombasa.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kupokea mashine hizo, Kaimu meneja mkuu anayesimamia masuala ya uhandisi katika bandari hiyo Javan Wanga amesema mashine hizo zitasaidia katika utendakazi wa bandari ya Mombasa.
Wanga hata hivyo amedokeza kwamba mashine hizo zilizo na uwezo wa kupakua makasha elfu 4 kutoka kwa Meli za kutoka mataifa mbalimbali zitaanza kazi rasmi mwezi Mei baada ya kukamilika kwa ujenzi wa eneo la kuegesha makasha.
Wakati uo huo amepongeza hatua ya ujenzi mpya wa eneo la pili la kuegesha makasha, akisema eneo hilo litachangia pakubwa katika kuboresha utendakazi wa bandari hiyo