Bodi ya utalii nchini imeandaa kongamano la wadau katika sekta ya utalii kutoka kaunti sita za Pwani kujadili changamoto zinazosibu sekta hiyo pamoja na mikakati ya kuimarisha sekta ya utalii.
Kongamano hilo linajiri tu baada ya wizara ya utalii nchini kuunda bodi ya utalii Pwani iliyopewa jukumu la kuhakikisha kuwa mbali na fuo za bahari kuwa vivutio vya utalii, bodi hiyo ya utalii Pwani imetwikwa jukumu la kutafuta vivutio vingine ambavyo vitavutia utalii.
Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo katiba katika wizara ya utalii nchini Joe Okuda kule Diani, Okuda amesema kuwa kongamano hilo linalenga kuainisha changamoto zinazosibu sekta ya utalii hasa katika fuo za bahari.
Okuda vile vile amesema kuwa sekta ya utalii nchini iliimarika kwa asilimia 37 mwaka 2018 ikilinganishwa na miaka ya hapo awali.
Taarifa na Salim Mwakazi.