Picha kwa hisani –
Chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT, kimedai kuwa kitawashinikiza wanachama wake kushiriki mgomo wa kitaifa.
KNUT imesema itachukua hatua hiyo baada ya kipindi cha siku 14 iwapo Tume ya kuajiri walimu nchini TSC, haitaanzisha mazungumzo kuhusu mkataba walioafikiana hapo awali wa maelewano wa CBA.
Katika taarifa iliotolewa na waziri wa Leba nchini Simon Chelugui, chama cha KNUT kimetoa makataa siku 14 kuwa watashiriki mgomo wa kitaifa iwapo serikali na Tume ya TSC hataangazia lalama zao basi walimu watashiriki mgomo wa kitaifa.
Hata hivyo kupitia Katibu wake mkuu, Wilson Sossion KNUT imesema Tume ya TSC, imekuwa iki kiuka sheria za Leba na kuendelea kuwakandamiza walimu kupata haki zao za kimsingi kwa mujibu wa mkabata wa CBA.