Picha kwa Hisani –
Chama cha walimu nchini KNUT kimeitaka tume ya kuajiri waalimu nchini TSC kuwaongeza mishahara sawa na kuwapandisha vyeo waalimu wa humu nchini ili kuwapa motisha zaidi wa kufanya kazi hio.
Akizungumza kwenye halfa ya maadhimisho ya siku ya waalimu ulimwenginu iliyoandaliwa jijini Nairobi,katibu mkuu wa chama hicho Wilson Sossion amesema ni kupitia kutimizwa kwa matakwa hayo ndipo fani ya ualimu itapata hadhi.
Sossion amesema kuwa iwapo waalimu hawatapewa motisha,ubunifu na mafanikio katika sekta ya elimu yatakua haba hali itakayorudisha nyuma viwango vya elimu nchini.
Kwa upande wake shirika la umoja wa mataifa la Elimu,sayansi na utamaduni UNESCO limetaka changamoto zinazokumba waalimu ikiwemo mishahara duni na kutopandishwa vyeo kusuluhishwa ili kuleta mafanikio katika sekta ya elimu.