Picha kwa hisani –
Chama cha waalimu nchini KNUT kimewataka walimu kuidhinisha mipangilio itakayohakikisha wanafunzi wote wa kike na wa wakiume wanahudhuria masomo punde shule zitakapofunguliwa.
Katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion amesema wanafunzi wamepitia changamoto wakati huu ambapo wamesalia nyumbani kwa mda mrefu ikiwemo kupata ujauzito ,na iwapo hawatofatiliwa huenda baadhi wakasitisha masomo yao.
Sossion vile vile amesema lazima kubuniwe kitengo cha kushughulikia dhulma za kijinsia katika shule zote za humu nchini ili kuhakikisha wanafunzi usalama wao,kwani takwimu zimedhihirisha kwamba wanafunzi wanapitia dhulma nyingi.
Amesema chama cha KNUT kitashirikiana na tume ya kuajiri waalimu nchini TSC na wakuu wa wizara ya elimu kuhakikisha wanafanikisha mchakato huo wa kushughulikia dhulma za kijinsia miongoni mwa wanafunzi.