Story by Our Correspondents –
Chama cha walimu nchini KNUT kimeitaka Tume ya kuajiri walimu nchini TSC kuhakikisha inaangazia malalamishi yalioibuliwa na Walimu kuhusiana na mpango wa kuendeleza masomo kwa walimu wa TPD.
Katibu mkuu wa Chama hicho Collins Oyuu amesema TSC haifai kupuuza lalama hizo za walimu huku akisisitiza haja ya Tume hiyo kuwajibikia swala hilo kwani ni sawa na kuwakandamiza walimu nchini.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya walimu duniani, Oyuu amesema ni lazima serikali kugharamia kora ya walimu katika mpango huo wa kuendeleza masomo ya walimu wa TPD kwani kwa sasa walimu wanapitia changamoto nyingi
Kwa upande wake Katibu mkuu wa Chama cha walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini KUPPET Akelo Misori ameitaka serikali kuangazia swala la uhaba wa walimu katika shule mbalimbali nchini.
Akijubu lalama hizo, Afisa mkuu mtendaji wa Tume ya kuajiri walimu nchini TSC Nancy Macharia, ameahidi kuangazia kwa kina maslahi ya walimu wote nchini kwani serikali haina nia mbaya kwa walimu.