Picha kwa hisani –
Katibu wa Chama cha Walimu nchini KNUT tawi la Kilindini Dan Aloo amesema ni lazima maswala msingi yazingatiwe kabla ya ufunguzi wa shule nchini.
Katika hotuba yake hapo jana Aloo amesema hakuna upanuzi uliofanyiwa shule za humu nchini wala kuajiriwa walimu zaidi akisema ni sharti mipangilio inayostahili iwekezwe.
Kulingana na Aloo, japo visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vimeanza kupungua nchini bado mazingira ya shule ni hatari kwa wanafunzi iwapo wataruhisiwa kuendelea na masomo.
Kauli yake imejiri huku Waziri wa Elimu nchini Profesa George Magoha akidokeza kuwa shule huenda zikafunguliwa mapema kabla ya mwezi Januari kama ilivyobashiriwa awali.