Picha kwa hisani –
Muungano wa wahudumu wa Afya nchini KMPDU umesema ifkikapo tarehe 7 mwezi huu wahudumu wafaya wataanza rasmi mgomo wao.
Katibu mkuu wa Muungano huo Daktari Chibanzi Mwachonda, amesema kwamba bado wanashikilia msimamo wao wa kushirikia mgomo iwapo matakwa yao hayatatekelezwa.
Mwachonda amesema wahudumu wa afya wanalalamikia mazingira duni ya utendakazi pamoja na kutojuimuishwa kwa tume ya huduma za afya katika mwada wa marekebisho ya katiba.
Mwachonda aidha ameelezea kwamaba japo serikali iliwapatia bima ya afya waliohitaji, bado kuna baadhi yao walioachwa nje ya bima hiyo, na sasa hawatakubali tena wahudumu wa afya waangamize maisha yao.