Picha kwa Hisani –
Muungano wa madaktari nchini KMPDU unapanga kufanya mkutano na wanachama wote wa muungano huo kote nchini hivi karibuni.
Katibu mkuu wa muungano huo Dkt Mwachonda Chibanzi amesema kwenye kikao hicho watajadili changamoto zinazowakumba wahudumu wa afya na kutoa mapendekezo kwa serikali ya jinsi wanavyotaka yasuluhishwe.
Chibanzi amesema wahudumu wa afya wataendelea kupigania kubuniwa kwa tume ya huduma za afya nchini akisema ni kupitia tume hio ndipo changamoto zinazowakumba wahudumu wa afya zitatuliwa.
Chibanzi amesema iwapo matakwa ya wahudumu wa afya yatakayowasilishwa kwa serikali hayatosuluhishwa kwa wakati watashinikiza wanachama wa muungano huo wa madaktari kote nchini kushiriki mgomo.