Katika jihudi za kukabili visa vya dhuluma za kijinsia katika kaunti ya Mombasa, sasa kituo maalum kitajengwa ili kuwanusuru wanaodhulumiwa.
Mwakilishi wa kike wa kaunti hiyo, Bi Asha Hussein amesema kwamba ni lazima wanawake na watoto wanaodhulumiwa wapewe hifadhi kadri idara ya usalama na vitengo vyengine husika vinapoziandama kesi hizo.
Bi Hussein amesema kwamba visa hivyo vya dhulma za kijinsia vinashuhudiwa kila uchao katika Kaunti hiyo japo wahanga wa dhuluma hizo husalia mitaani badala ya kuwa katika maeneo salama.
Kiongozi huyo amesema kwamba tayari harakati hizo zimeanzishwa ili kuwalinda wale wanaodhulumiwa sawa na kuhakikisha wanapata haki kupitia kwa idara ya mahakama.