Mkurugenzi wa kituo cha kiteknolojia na sanaa cha SwahiliPot-Hub mjini Mombasa Fatma Mkwariza amesema kuidhinishwa kwa kituo hicho kwa kiwango kikubwa kimewaepusha vijana wengi na maovu katika jamii.
Fatma anasema vijana wengi wamekuwa wakijisajili na kituo hicho ili kukuza talanta zao na kujiendeleza katika maswala ya kiteknolijia hali ambayo imewaondoa katika hatari ya kupotoka kimaadili.
Fatma amehoji kuwa eneo la Pwani linashuhudia tatizo la utumizi wa dawa za kulevya sawa na itikadi kali na kituo hicho kimekuwa na umuhimu katika kumkinga kijana na maovu hayo.
Hata hivyo amefichua kuwa vijana wengi waliyokuwa katika hatari ya kusajiliwa katika makundi ya kihalifu hasa katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya Mombasa sasa wameingilia kikamilifu sanaa.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.