Story by Our Correspondents –
Wizara ya Afya nchini imefungua rasmi kituo cha kisasa cha kutibu ugonjwa wa Saratani katika hospitali kuu ya kanda ya Pwani wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya kimataifa ya ugonjwa wa Saratani.
Akihutubia Wanahabari baada ya kufungua rasmi kituo hicho katika halfa iliyohudhuriwa na Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho, Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe amesema kituo hicho kitasaidia pakubwa kukabiliana na ugonjwa wa saratani.
Kagwe amedokeza kwamba kituo hicho kitapunguza gharama ya matibabu ya wagonjwa wa saratani kwani wengi wao walikuwa wakilazimika kusafari hadi jijini Nairobi na hata nje ya nchi kutafuta matibabu ya ugonjwa wa Saratani.
Kwa upande wake Gavana wa Mombasa Hassan Ali Joho amesema kituo hicho kitasaidia pakubwa familia za watu wanaokabiliwa na ugonjwa wa Saratani katika kupata matibabu.