Kituo cha habari cha Radio Kaya kwa ushirikiano na wadau mbalimbali kimezikidhi kwa chakula zaidi ya familia 25 za watu wanaokabiliwa na ugonjwa za ukoma katika kijiji cha Tumbe eneo la Msambweni kaunti ya Kwale.
Menaja wa Kituo cha habari cha Radio Kaya Victor Ongwena amesema hatua hiyo ni kutokana na wito wa serikali kwa wahisani mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia watu wanaopitia changamoto za ukosefu wa chakula wakati huu wa janga la Corona.
Victor amesema mpango huo utaendelezwa ili kuhakikisha jamii mbalimbali zinazohitaji msaada wa chakula zinawezeshwa wakati huu mgumu, huku akiwasihi wahisani kujitokeza na kuzisaidia jamii zisizojiweza.
Kwa upande wake Mwanaharakati wa kijamii George Jaramba amesema zoezi hilo linafaa kuendelezwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali kwani serikali pekee haiwezi kukidhi familia zote zinazokabiliwa na changamoto.
Hata hivyo Familia hizo zikiongozwa na Bekisubu Kisubi Dziya zimekishukuru Kituo cha habari cha Radio Kaya kwa ushirikiano na wadau mbalimbali kwa kuwasaidia kwa chakula hicho, huku wakiwaomba wahisani mbalimbali kujitokeza na misaada mbalimbali.