Story by Gabriel Mwaganjoni –
Jumla ya watu 365 wameaga dunia kutokana na makali ya virusi vya Corona katika kaunti ya Mombasa tangu mwaka uliyopita.
Kamishna wa kaunti hiyo Gilbert Kitiyo amesema takwimu hizo zimepelekea mikakati muafaka kuidhinishwa kwa lengo la kudhibiti maambukizi zaidi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuwahamasisha wakaazi kuhusu umuhimu wa kujikinga na Corona katika hafla iliyofanyika katika bustani la Treasury mjini Mombasa, Kitiyo amewakosoa wanasiasa kwa kuendeleza siasa zao bila ya kuzingatia masharti ya kudhibiti maambukizi.
Afisa huyo tawala hata hivyo amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kuzingatia kikamilifu masharti ya kudhibiti msambao wa virusi vya Corona.