Story by Our Correspondents-
Huenda wakaazi wa kaunti ya Kilifi wakanufaika kimaendeleo iwapo watawachagua viongozi waadilifi na wenye malengo ya maendeleo.
Ni kauli iliyotolewa na Mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Kilifi Wakili George Kithi aliyesema maendeleo hayo yataafikiwa kupitia uongozi wake iwapo wakaazi wa kaunti hiyo wataunga mkono azma yake ya ugavana.
Akizungumza katika mikutano yake ya kisiasa katika kaunti hiyo Wakili Kithi amesema punde tu atakapochukua serikali ya kaunti ya Kilifi baada ya uchaguzi atatenga shilingi milioni 600 kujenga kiwanda cha mnazi katika kaunti hiyo ili kubuni ajira.
Hata hivyo amedokeza kwamba yuko tayari kushirikiana na wakaazi wa kaunti ya Kilifi ili kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inafanikishwa.