Picha kwa hisani –
Maafisa wa polisi kaunti ya Kisii wamemtia nguvuni naibu gavana wa kaunti hio Joash Maangi pamoja na mbunge wa Mugirango kusini Slyvanus Osoro.
Wawili hao wametiwa nguvuni wakati wakisubiri kumpokea naibu wa rais William Ruto ambae amehudhuria ibada ya mazishi ya mwendazake simeon Nyachae katika uwanja wa Gusii kaunti ya Kisii.
Ripoti zimeeleza kwamba maafisa wa polisi wamewashurutisha viongozi hao kuingia katika gari la maafisa wa idara ya DCI kabla ya gari hilo kupelekwa kwa kasi hadi katika makao makuu ya idara ya DCI ambako wanahojiwa.
Polisi hawajatoa maelezo yeyote kuhusu chanzo cha kutiwa nguvuni kwa wawili hao ambao walikua wanahudhuria ibada ya mazishi ya Simeon Nyachae.