Picha kwa hisani –
Machifu katika Gatuzi dogo la Kisauni Kaunti ya Mombasa wametakiwa kukabiliana na biashara ya pombe haramu katika eneo hilo.
Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo amesema licha ya pombe haramu kuuzwa katika kila pembe ya eneo hilo la Kisauni, Machifu wamepuuza hali hiyo na kuichukulia kama ya kawaida.
Kitiyo ameonya kwamba biashara hiyo ya pombe haramu imechangia utovu wa usalama katika eneo hilo la Kisauni.
Wakati uo huo, Kitiyo amewataka machifu kuwajibika ili kutoa muongozo unaostahili kwa jamii ya eneo hilo la Kisauni.
Kitiyo aidha amewatahadharishwa maafisa hao tawala dhidi ya kushiriki siasa akisema hali ya Maafisa hao kuchukua mirengo ya kisiasa kutapelekea kushindwa a kutekeleza jukumu lao la kuimarisha usalama mashinani.