Bingwa wa mbio za marathon na Mwanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge ameshinda mbio za kilomita 42.2 za NN Mission Marathon zilizoandaliwa katika uwanja wa ndege wa Twente nchini Uholanzi.
Kipchoge amekimbia mbio hizo kwa mda wa 2:04:38 huku nafasi ya pili ikishikiliwa na mkenya Jonathan Korir aliyekimbia kwa mda wa 2:06:04
Mshindi wa tatu katika mbio hizo ni Goitom Kifle ambaye ni mzaliwa wa taifa la Eritrea na amekimbia kwa mda wa 2:08:04.
Mbio hizo zimeandaliwa kabla ya mashindano ya Olympic Toyko mwaka wa 2020 ambazo zitaandaliwa nchini Japan mwezi Julai na Agosti.