Picha kwa Hisani –
Kiongozi wa mashatka ya umma nchini Noordin Haji ameagiza kukamatwa kwa aliyekuwa mkurungezi wa Mamlaka ya Bandari Daniel Manduku kwa matumizi mabaya ya shilingi milioni 244.
Baada ya kufanya uchunguzi afisi ya kiongozi huyo wa mashtaka imebaini kwamba mamlaka ya Bandari iliweza kufanya malipo ya zaidi ya shilingi milioni 244 kwa wanakanadarasi kwa kazi ambayo hawakukamilisha.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari mapema leo, Haji amesmea kuna ushahidi wa kutosha dhidi ya aliyekuwa mkurungezi pamoja na afisa wa mamlaka hiyo Juma Chigulu.