Picha kwa hisani –
Kiongozi Mkuu wa kidini nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameweka ujumbe mtandaoni akitoa wito Donald Trump ashambuliwe kama hatua ya kulipiza kisasi ya mauaji ya komanda wa juu wa jeshi, Jenerali wa kikosi maalum cha Iran Qasem Suleimani.
Picha kwenye tovuti yake rasmi inamuonesha aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump akicheza gofu katika kivuli cha ndege ya kivita au ndege kubwa isiyo na rubani.
Mtandao wa Twitter hata hivyo umefunga akaunti ambayo ilikuwa ya kwanza kuweka picha hiyo.