Story by Mimuh Mohamed–
Mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinywa ameongoza kikao maalum cha kupanga mipangilio ya hafla ya kukabidhiana mamlaka ya urais wakati huu ambapo muda wa tume ya IEBC kutangaza matokeo ya urais unazidi kukaribia.
Akizungumza katika jumba la Harambee jijini Nairobi wakati wa kikao cha kamati maalum ya kuchukua madaraka ya ofisi ya rais, Kinyua amesema kamati hiyo imejipanga kuhakikisha makabidhiano ya mamlaka kutoka kwa rais wa sasa hadi rais anayeingia yanafanyika vyema.
Rais wa sasa Uhuru Kenyatta awali alichapisha katika gazeti rasmi la serikali orodha ya maafisa watakao keti katika kamati hiyo, itakayosaidia kukabidhiwa mamlaka kwa rais mteule na kumkabidhi maelezo ya usalama pamoja na ushauri.
Wanachama wa kamati hiyo ni pamoja na Joseph Kinyua, Fred Matiang’i, Karanja kibicho, Insepkta jenerali Hillary Mutyambai, mkuu wa majeshi nchini jenerali Robert Kibochi, Mkuu wa kitengo cha ujasusi Philip Kameru, makatibu wa kudumu Julius Korir na Joe Okudo.
Wengine ni makatibu wa kudumu Jerome Ochieng, Julius Muia, Macharia Kamau, Wakili mkuu wa serikali Ken Ogeto, mwanasheria mkuu Paul Kihara, msajili wa mahakama Anne Amadi na Kinuthia mbugua.
Tume ya IEBC na idara ya mahakama pia zinahusika na kukabidhiana mamlaka ya rais.