Nyimbo mpya ya mwanamuziki nyota wa bongo flava kutoka Tanzania, Ali Kiba kwa jina ‘Dodo’ umezua hisia tofauti tofauti baada ya kumshirikisha aliyekuwa mke wa zamani wa Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto kama mke wake na anamvisha pete katika video ya wimbo huo.
Mwanamuziki na mfanyibiashara huyo Hamisa Mobetto ameonyesha urafiki wake kwa Ali Kiba ambaye anakadiriwa kutoelewana na mzazi mwenzake Diamond kwa miaka sasa. Wawili hao waliweza kuiweka kazi yao kama siri kwani hakukuwa na tetesi yoyote ya kazi hiyo kabla ya kuachiliwa kwa ngoma hii tarehe saba ya mwezi huu. Katika mahojiano na kituo kimoja cha radio huko Tanzania, Ali Kiba alisema kuwa mbali na uzuri wa nyimbo yake na uzuri wa video hiyo, lipo jambo ambalo ana imani nalo kuwa litafanya nyimbo hiyo kuzungumziwa sana.
Ushirikiano huo unajiri wiki chache tu baada ya tetesi kuwa Hamisa na Diamond wamerejea kwenye mahusiano ya kimapenzi baada ya Diamond kupost video ya Hamisa akicheza wimbo wake ‘Jeje’
Mashabiki wa wawili hao wameelezea kupitia mitandao ya kijamii kuwa hawakutarajia, wengine wakiwakashifu kwa jambo hilo wakilitaja kama hatua ya kuuza wimbo huku wengine wakipongeza kwa kushirikiana na kuwaunganisha mashabiki wao.
Unalizungumziaje swala hili?