Picha Kwa Hisani
Mwanamuziki Kennedy Ombima maarufu kama King Kaka ameeleza kwamba amekuwa akiugua kwa muda usiopungua miezi mitatu.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, King Kaka amefichua kuwa hajakuwa na hisia ya ladha kwa kipindi cha miezi miwili na amekuwa akila matunda na kunywa uji tu.
Msanii huyo anayefahamika sana kwa kibao chake ‘Wajinga nyinyi’ amesema kuwa madaktari walikosea katika kutambua anachougua na katika kipindi hicho amepoteza kilo 33 na kiuno chake kimepungua na inchi tatu.
Mwanamuziki huyo ana mkusanyiko wa nyimbo ambazo alirekodi kabla ya kugonjeka na anasema ameamua kuuita “Happy Hour” kutokana na aliyopitia kwa miezi mitatu sasa.
Aidha, King Kaka anaamini ataibuka mshindi dhidi ya kinachosibu afia yake. Tunamtakia King Kaka afueni ya haraka.