Aliyekuwa Kinara wa shughuli za bunge la Kaunti ya Mombasa Charles Kitula amebanduliwa nje ya afisi hiyo.
Kitula ambaye ni Mwakilishi wa Wadi ya Freere town katika bunge la Kaunti ya Mombasa amenyang’anywa wadhfa huo ambao umekabidhiwa Mwakilishi wa Wadi ya Chaani Junior Wambua.
Hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kutokana na kubanduliwa nje kwa Kitula japo Kiongozi huyo katika siku za hivi majuzi ameonekana kumpinga vikali Gavana wa Kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho.
Kitula amekuwa akimkosoa Joho kwa ubaguzi katika ugavi wa fedha za basari akidai fedha hizo zinatolewa kiubaguzi huku baadhi ya Wadi ikiwemo yake ya Freere town eneo bunge la Nyali zikiwachwa nje ya mgao huo.