Picha Kwa Hisani –
Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga apuuzilia mbali madai yaliyotolewa na Naibu wa Rais William Ruto kuwa kuna kundi lenye ushawishi mkubwa ambalo linapanga kuiba kura katika uchaguzi ujao ili kumzuia kuingia Ikulu.
Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa maafisa wapya wa bodi ya uchaguzi ya chama cha ODM hapo jana, Odinga amesema wananchi ndio uchagua kiongozi wanaemtaka akitaja madai hayo kama yasiokua na msingi.
Odinga aidha ameweka wazi kuwa mchakato wa BBI bado ungalipo akisema kura ya maamuzi ya kufanyia marekebisho katiba ya nchi itaandaliwa kabla ya uchuguzi mkuu ujao.