Picha kwa Hisani –
Ni sharti rais Uhuru Kenyatta afikirie kuhusu uchumi wa nchi ambao umesambaratishwa na makali ya janga la Corona.
Haya ni kulingana na kinara wa Chama cha WIPER Stephen Kalonzo Musyoka ambae amesema taifa limetikishwa kiuchumi na janga laCorona na ni sharti mbinu za kuufufua uchumi wa nchi zitiliwe mkazo.
Kalonzo amemsihi rais Kenyatta kufufua uchumi ili Wakenya hasa vijana wanufaike na nafasi za ajira na za kibiashara.
Wakati uo huo Kalonzo amemtaka kiongozi wa nchi kutoulegezea kamba ufisadi unaozidi kulididimiza taifa.