Idara ya utabiri wa hali ya anga, imeweka wazi kuwa hali ya ukavu na joto jingi itazidi kushuhudiwa ndani ya wiki mbili zijazo.
Mkurugenzi wa Idara hiyo kaunti ya Kwale, Dominic Mbindio amesema upepo unaosababisha mvua umechelewa kutokana na kimbunga kwa jina Idai kinachoshuhudiwa kwenye bahari ya Madagascar.
Akizungumza na Mwanahabari wetu, Mbindio amesema kimbunga hicho kimechelewesha upepo wa kusi kufika Afrika Mashariki.
Mbindio hata hivyo amesema wakulima hawafai kufa moyo kwani upepo unaosababisha Mvua umefika sehemu za Tanzania, akihoji kuwa msimu wa Mvua ya Masika unatarajiwa kuanza baada ya kimbunga hicho kuisha.
Taarifa na Dominick Mwambui.