Shule moja ya msingi ya Girimacha eneo la Malanga imepata hasara ya tarkriban shilingi laki moja na nusu baada ya kimbunga kikali kulingoa paa la darasa moja la shule hiyo.
Shule moja ya msingi ya Girimacha eneo la Malanga imepata hasara ya tarkriban shilingi laki moja na nusu baada ya kibunga kikali kulingoa paa la darasa moja la shule hiyo usiku wa kuamkia leo.
Mwenye kiti wa shule hiu Kitsao Birya anasema upepo mkali umeshughudiwa katika eneo hilo hali iliyopelekea kuzuka kwa kimbunga hicho kilichosalia hasara hiyo.
Birya amesema Kimbunga hicho kimetokea usiku na pia kulingoa paa la jiko huku wanafunzi wakiwa katika likizo yao ya mwezi wa nane.
Mwenyekiti huyo Sasa amesema kuwa kama kamati ya shule watafanya mikakati ya haraka ili kuona kwamba darasa hilo moja pamoja na jiko linakarabatiwa kabla ya wanafunzi kufungua rasmi.
Taarifa na Charo Banda.