Picha Kwa Hisani
Story by: Charo Banda
Hali ya wasi wasi imetanda katika eneo mbogolo kule Ganda – Malindi Kaunti ya Kilifi baada ya watu wawili kuuwawa kinyama na miili yao kutupwa kwenye mto.
Akithibitisha tukio hilo Naibu Chifu wa Ganda Hassan Mazoa amesema wawili hao wameaga dunia baada ya kupigwa na umati wa watu wakituhumiwa kwa wizi wa mbuzi.
Baadhi ya wakaazi wa eneo hilo hata hivyo wametilia shaka iwapo wawili hao walijihusisha na wizi wa mifugo hio kama inavyodaiwa.