Picha kwa hisani –
Bunge la Seneti limehairisha tena kikao cha kujadili mswada wa mfumo mpya wa ugavi wa mapato kwa serikali za kaunti baada ya maseneta kupiga kura ya kusitisha kujadiliwa kwa mswada huo bungeni.
Maseneta hao wamepiga kura kwa idadi 34 dhidi ya 26, huku mmoja kati yao akikosa kupiga kura na kupelekea Spika wa bunge hilo Ken Lusaka akaamua kuhairisha kujadiliwa kwa mswada huo bungeni.
Hatua hiyo imeafikiwa baada ya Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen kuzua hoja bungeni kwa kutumia kipengele cha 105 cha hoja za bunge na kuwashinikiza wabunge kupiga kura ya kuhairishwa kwa kikao hicho bungeni.
Hata hivyo baada ya mswada huo kuekwa kando bungeni, Seneta wa Bungoma Moses Wetangula ametoa falsafa bungeni kwa kunakili kitabu kilichoandikwa na muandishi mmoja kutoka taifa jirani la Tanzania kinachozungumzia kuhusu swala la uongozi.