Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.
Familia moja kutoka Jijini Nairobi inaomba kusaidiwa kumpata kijana wao aliyetoweka mjini Mombasa takriban majuma mawili yaliyopita.
Kulingana na mjombake kijana huyo Gilbert Oguro, binamu yake Jeff Omondi alisafiri kutoka Jijini Nairobi hadi Mombasa tarehe 10 mwezi huu ili kukutana na dadake japo wawili hao hawakukutana.
Oguro amesema licha ya familia hiyo kuripoti katika kituo cha polisi cha Central mjini Mombasa, bado haijafaulu kumpata jamaa yao huku simu yake ikiwa imezimwa tangu siku ya safari.
Oguro amesema familia hiyo imekabiliwa na mahangaiko na mateso mengi ya kisaikolojia ikiwaomba wakaazi wa eneo la Pwani walio na ufahamu kumhusu Omondi waisaidie familia hiyo kumpata jamaa wao.