
Familia ya marehemu.
Kijana mmoja ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa maafisa wa polisi katika eneo la Bondeni Kaunti ya Mombasa adhuhuri ya leo.
Haijabainika wazi sababu za mauaji hayo, japo Maafisa wa usalama hawajafichua lolote kuhusu tukio hilo.
Mashirika ya utetezi wa haki za kibinadamu la MUHURI na lile la Haki Afrika yamezuru eneo la mkasa wakitaka kubaini kiini cha mauaji hayo.
Afisa wa maswala ya dhaura katika Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu Haki Afrika Mathias Hezron Shipetta amesema kwamba tayari amewasilisha tukio hilo kwa tume inayochunguza maswala ya polisi nchini IPOA ili kubaini kiini cha tukio hilo.
Familia ya marehemu vile vile haijaongea lolote kuhusiana na tukio hilo, huku mwili wa marehemu Shee Hassan Adoli aliyekuwa na umri wa miaka 25 ukipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani.
Taarifa na Radio Kaya.