Hali ya huzuni imetanda katika uwanja wa michezo wa Alaskan mjini Malindi baada ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 23 aliyekuwa amejitokeza kwenye usajili wa makurutu kufariki wakati wa zoezi hilo.
Akithibitisha kisa hicho afisa mkuu aliyekuwa akisimamia zoezi hilo Luteni Kanali Joseph Nzioka amesema kuwa kijana huyo alishiriki mazoezi makali kabla ya kukimbia yaliyopelekea kuzirai na kushindwa kumaliza mbio hizo.
Luteni Nzioka aidha amesema kuwa maafisa wa matibabu katika jeshi wamejaribu kumfanyia huduma ya kwanza na kumkimbiza hospitali kuu ya Malindi ambapo amefariki.
Hata hivyo amewataka makurutu wanaolenga kujiunga na jeshi kuhakisha kuwa wanafanya mazoezi yakutosha kabla ya kujitosa katika zoezi la kutafuta kazi hiyo ya jeshi.
Kwa sasa mwili ya mwendazake unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Star mjini Malindi.
Taarifa na Charo Banda.