Kijana mmoja mwenye umri wa makamo kutoka eneo la Mkangagani kata ya Mida Majaoni amethibitishwa kufariki baada ya kupigwa kwa manati ( Panda) na mwenzake kichwani.
Inadaiwa kuwa kijana huyo kwa John Ndodo alikua katika eneo la kubugia mnazi na wenzake wakati ugomvi ulipozuka baina yake na jamaa mmoja kwa jina Kalume Chengo ambaye anadaiwa kumpiga kwa kifaa hicho kichwani na kumwacha hoi.
Akithibitisha kisa hicho naibu chifu wa kata ndogo ya Mida –Majaoni Renson Baya amesema kuwa kijana huyo amekimbizwa katika hospitali kuu ya Pwani ambapo amefariki wakati akipokea matibabu.
Baya aidha amesema kuwa tayari kijana aanayedaiwa kutekeleza kisa hicho ametiwa mbaroni na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Watamu huku uchunguzi ukianzishwa.
Taarifa na Charo Banda.