Hakimu mkuu wa mahakama ya Mombasa Julius Nang’ea amesema kuwa idara ya mahakama katika kaunti hio itatumia kikamilifu adhabu ya huduma za kijamii, ili kupunguza msongamano wa wafungwa katika magereza.
Nang’ea amesema adhabu hii inapaswa kuzingatiwa kwani baadhi ya watu huhukumiwa kwa kutekeleza makosa madogo yanayoweza kurekebishwa kupitia kifungo cha nje.
Hakimu huyo mkuu wa mahakama ya Mombasa hata hivyo amesema kwamba kifungo cha nje kinaweza kutolewa kwa watu wanaohukumiwa kifungo cha miaka mitatu kurudi chini na kuzingatia vipengele kama ukongwe, maradhi, mtoto au mwanafunzi
Taaria na Gabriel Mwaganjoni.