Msanii Kidis The Jembe rasmi amegeukia mziki wa gospel.
Kidis amekuwa na wakati mgumu kurudi katika ulingo wa burudani baada ya kuvuma na kibao Kamua Leo.
Kamua leo ilipata umaarufu zaidi pale alipokuwa chini ya lebo ya GrandPa. Hii ni baada ya wasanii Ameleena, Wyre, na DNA kushirikiana naye katika wimbo huo ambao awali ulikuwa ni kolabo kati ya Chapatizo na Kidis.
Akishirikiana na Mr Boo wakati huu Kidis amekuja kali na kibao kiitwacho utabarikiwa.
Huyu ni msanii wa pili kutoka Pwani kuvuka ukuta na kuingia katika mziki wa injili. Msanii mwingine aliyejitosa katika injili ni Cannibal.
Tazama wimbo huo hapa.