Story by Janet Shume-
Kikosi cha kwanza cha wanajeshi kutoka humu nchini kilichoko chini ya kikosi cha Jumuiya ya afrika mashariki kimesafari nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ili kusaidia kuimarisha usalama eneo hilo.
Akizungumza katika hafla ya kuaga kikosi hicho kabla ya kusafiri kuelekea nchini Congo iliyofanyika katika eneo la Embakasi, mkuu wa majeshi nchini Jenerali Robert Kibochi amewahimiza wanajeshi hao kudumisha nidhamu pamoja na kutekeleza majukumu yao inavyotakikana.
Akisema hatua hiyo itasaidia katika kuimarisha uhusiano mwema wa kidiplomasia pamoja na kisiasa kati ya Kenya na Congo.
Itakumbukwa kwamba siku ya Jumatano, bunge la kitaifa lilipitisha hoja ya maafisa wa kikosi cha ulinzi cha KDF kutumwa mashariki wa Congo kusaidia katika kutekeleza operesheni ya kiusalama.