Picha kwa hisani –
Katibu katika Wizara ya usalama wa ndani Dkt Karanja Kibicho ameandikisha taarifa kwa idara ya upelekezi wa jinai nchini DCI kuhusu madai yaliyoibuliwa na aliyekuuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko ya kupanga vurugu wakati wa uchaguzi mkuu 2017.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuandikisha taarifa kwa idara hiyo, Kibicho amesema Sonko atachukulia hatua kali za kisheria kwa madai ya kumharibia jina.
Kibicho amesema tangu Sonko aondolewe Madarakani imekuwa akiwaharibia watu majina kwa kuibua madai yasiokuwa na msingi wowote huku akisema ni lazima Sonko atoa maelezo zaidi sawia na kuwajibikia madai anayoyazua.
Inadaiwa kuwa Sonko alisema Serikali ilipanga na kufadhili vurugu kwa usimamizi wa Kibicho ili kuhujumu kampeni za chama cha ODM za kuwania kiti cha urais mwaka wa 2017.