Story by Gabriel Mwaganjoni –
Licha ya elimu ya umma kutolewa kwa wananchi kuhusu athari za ukabila wakati wa uchaguzi mkuu, idadi kubwa ya wananchi bado wameshikilia kigezo cha ukabila katika kuwachagua viongozi wao.
Hayo ni kulingana na Mwenyekiti wa Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la MUHURI, Khelef Khalifa aliyesema ukabila umesambaratisha uongozi, uiano na maendeleo nchini huku wale wanaoingia uongozini wakiyahudumia makabila yao pekee.
Khalifa hata hivyo amesema ni sharti elimu ya umma itolewe mashinani kuhusu swala la uchaguzi ili wananchi wabadili mbinu ya kuwateua viongozi wao.
Wakati uo huo, amedokeza kwamba ukosefu wa uwazi katika zoezi la kura kila baada ya kipindi cha miaka mitano umechangia chuki na mfarakano miongoni mwa wananchi.