Picha kwa Hisani –
Rapper Khaligraph Jones kutoka Nairobi amezua gumzo mtandaoni baada ya kushindwa kujizuia na kufunguka hadharani kupitia mtandao wa Instagram jinsi anavyomkubali msanii wa muziki wa kizazi kipya Adasa.
Adasa ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya alichomshirikisha na rapper Benzema kwa jina ‘Najikakamua’, anauwezo mkubwa wa sauti na amekua akitikisa mawimbi ya radio na televisheni nchini Kenya kwa muda sasa.
“Wale wanasemanga Kenya Hakuna Talent, This lady Has one of the Best Voices in Africa and Probably the Best voice In East Africa, Tusibishane Tafadhali, This song is beautiful, Her name is @officialadasa , Kama kitu Ni noma , ni noma #respecttheogs,” aliandika Khaligraph Jones kupitia Instagram yake.
Wasanii wengine kutoka Nairobi wakiwemo Prezzo, Sauti Sol, Magix Enga na wengine wengi wamekubaliana moja kwa moja na kauli ya OG kuwa Adasa anakipaji cha kipekee na huenda akawa hana mpinzani si hapa Afrika mashariki pekee bali Afrika nzima kama alivyonukuu Khaligraph Jones akitoa hisia zake za ndani.
Kupitia Instagram, Khaligraph Jones amejitoa kimasomaso kuzi pandisha kazi mbili za Adasa ‘Tunaendana’ na hii mpya kwa jina Tujikakamue aliyomshirikisha rapper Benzema .