Bodi ya filamu nchini yaani ‘KFCB’ imeitaka idara ya usalama katika ukanda wa Pwani kushirikiana na bodi hiyo ili kuimarisha usalama katika maeneo ya baharini kipindi hiki cha sherehe za mwisho wa mwaka.
Akiongea mjini Mombasa Afisa mkuu wa bodi hiyo kanda ya Pwani, Boniventure Kioko amesema kuwa idadi ya watalii inatarajiwa kuongezeka na kuna haja ya usalama kuimarishwa ili kuhakikisha visa vya utovu wa kiusalama havishuhudiwi.
Hata hivyo amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao,akisema kuwa mara nyingi watoto wakike upata mimba huku vijana wakijiingiza kwenye utumizi wa mihadarati msimu huu wa sherehe za mwisho wa mwaka.
Wakati uo huo amesema bodi hio imetoa mafunzo kwa baadhi ya makundi ya vijana watakaosaidia kutoa ripoti kuhusu visa vya dhulma watakavyovishuhudia hususani katika fukwe za bahari.
Taarifa na Hussein Mdune.