Story by Charo Banda-
Kesi iliyowasilishwa katika Mahakama kuu ya Malindi ya kupiga ushindi wa Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro imeanza rasmi.
Jaji wa Mahakama hiyo Ann Adwera amesema tayari mashahidi wanne ambao walikuwa ni maajenti wa chama cha PAA wamejitokeza kutoa ushahidi wao dhidi ya kesi hiyo wakiongozwa na Mtana Sang aliyekuwa ajenti mkuu wa kituo cha kupiga kura cha Garashi.
Akitoa ushahidi wake mbele ya Mahakama hiyo, shahidi wa kwanza katika kesi hiyo Mtana Sang ameiambia Mahakama kwamba maafisa wa IEBC walishindwa kufanya majukumu yao na kumfanyia kampeni gavana wa Gideon Mung’aro.
Sang vile vile ameiambia Mahakama kwamba maajenti wa chama cha PAA hawakuruhusiwa kusalia ndani ya kituo cha kujumlisha na kuhesabu kura baada ya wananchi kupiga kura kwani walitimulia na maafisa wa IEBC.
Hata hivyo Jaji wa Mahakama hiyo Ann Adwera apinga ombi la Gavana Mung’aro la kuitaka Mahakama kuiondoa kesi hiyo, akisema ushahidi uliyowasilishwa Mahakamani una uzito wa kuchangia kesi hiyo kuendelea kusikizwa.
Jaji Adwera, amesema Mahakama itawapa nafasi wale wote wanaohusika katika kesi hiyo ikiwemo walalamishi ambao ni pamoja na Justine Ringa, Justine Charo na Salim Chai pamoja na upande wa Gavana Mung’aro na Tume ya IEBC kabla ya uamuzi kutolewa.