Wawakilishi wa Kenya katika mashindano ya COPA Cocacola Afrika Cup Of Nations, St Anthony’s wameichabanga Ethiopia mabao 11-1 katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa katika shule ya upili ya Nakuru.
Fred Kendigi aliipa Kenya uongozi katika dakika ya tatu, Issa Rashid akaongeza la pili katika dakika ya 12, kisha akaongeza la tatu katika dakika ya 21.
Katika kipindi cha pili Daniel Odhiambo ameifungia Kenya la nne. Katika dakika ya 52 Kendigi alivurumisha tena kombora, Rashid naye akadumbuizwa lingine dakika ya 50.
Ethiopia walipata la kufutia machozi kupitia Tsegaye Dawit. Jambo lilowakasirisha wachezaji wa Kenya na kuongeza kibano dhidi ya Ethiopia. Jacob Onyango akafunga mawili, Harun Kibiwot na Onyango wakaongeza mengine tena.
Kenya wanakutana na Botswana siku ya Jumatano.