Picha kwa Hisani –
Chama cha madaktari wanaoshughulikia maradhi ya moyo nchini yaani Kenya Cardiac Society kimesema asilimia 12 ya vifo vinavyoshuhudiwa nchini vimechangiwa na maradhi ya moyo.
Kulingana na Lilian Mbau mmoja wa madaktari katika chama hicho,ugonjwa wa moyo umeathiri wakenya wengi, kwani asilimia 25 ya wagonjwa wanaolazwa katika vituo vya afya nchini wanakabiliwa na ugonjwa huo.
Daktari Mbau vile vile amesema licha ya kwamba wakenya wengi wanaugua ugonjwa wa moyo,wataalam wa kushughulikia maradhi hayo ni wachache na wananchi wa mashinani hawapati huduma kutoka kwa wataalam hao.
Chama hicho cha wataalam wa ugonjwa wa moyo nchini hata hivyo kimewataka wakenya kuzingatia lishe bora ili kuepuka maradhi hayo.