Picha kwa hisani –
Kenya hii leo inaungana na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya maambukizi ya virusi vya HIV duniani.
Siku hii huadhimishwa kila mwezi wa Disemba mosi ili kuonyesha umoja kwa kuwasaidia watu walioathirika na virusi vya Ukimwi sawia na kukumbuka wale waliopoteza maisha yao kutokana na ugonjwa huo.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa António Guterres, amesema afya ni haki ya kila mtu na ni lazima ipewe kipaumbele katika uwekezaji na kuhakikisha afya bora kwa wote.
Kwa upande wake Mama wa taifa Bi Margaret Kenyatta, amesema kuna haja ya hamasa zaidi kufanywa kwa vijana humu nchini, ili kupunguza maambukizi na kuwakinga wale wanaoishi na virusi vya HIV kutokana na unyanyapaa.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni mshikamano wa kimataifa na uwajibikaji wa pamoja.